RAMANI YA UWANJA MPYA WA MPIRA WA GEITA GOLD FC

1. Ramani ikionesha muonekano wa uwanja wa Geita Gold FC baada ya kukamilika, ambapo halmashauri imetenga jumla ya ekari kumi, 10.4 (104,570 square mita za mraba ) kwaajili ya ujenzi wa uwanja huo wa kisasa wa michezo.

2. Uwanja huu ukikamilika utakuwa na uwezo wa kubeba jumla ya watazamaji elfu kumi na mbili (12000) wote wakiwa wamekaa, utakuwa na sehemu kiwanja cha mpira wa miguu, michoro ya sehemu za kukimbilia (riadha) pamoja na miundombinu mingine ikiwemo maeneo ya biashara na maegesho ya magari.

3. Uwanja huu utajengwa kwa kipindi cha miezi minne (4) na mradi wa ujenzi huu utagharimu jumla ya shilingi bilioni mbili (2,040,312,754.92), fedha ambazo zimetolewa na Kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Geita (GGML) ambao ndio wafadhili wa mradi huu.

4. Uwanja huu utajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakamilika ndani ya kipindi cha miezi minne tangu kusainiwa kwa mkataba huu (tarehe 2/07/2021mpaka 2/10/2021).

Geita Gold FC, The pride of Geita.

No comments