TFF WAMUONYA HUSSEIN BASHE
Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kushikitishwa na kauli ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe kuhusu matokeo ya mechi ya Simba na Yanga.
Kupitia mtandao wake wa kijamii, Naibu Waziri alidai waamuzi wa mechi hiyo walidhibitiwa, vinginevyo wangetoa adhabu ya penalti dhidi ya Yanga TFF inawaomba viongozi kuacha hisia zinazoweza kuchochea vurugu kwenye mpira wa miguu, na badala yake wahubiri amani.
Viongozi wana wajibu wa kuonesha uongozi kwa wanaowaongoza kwa kuwa makini na kauli zao.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ilimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0.
(Via;TFF)
Post a Comment