TFF WAMPONGEZA RAIS SAMIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwa miongoni mwa maelfu ya washabiki waliofika uwanjani kushuhudia mechi ya Simba na Yanga.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ilichezwa jana Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na Yanga kushinda bao 1-0.
Ujio wa Rais Samia uwanjani unadhihirisha kwa vitendo kuwa yeye ni mpenzi wa mpira wa miguu.
Hivi karibuni Rais Samia alitangaza kuondoa kodi kwenye nyasi bandia ambazo zinaagizwa kutoka nje ya nchi.
Hatua hiyo ni moja ya mikakati ya Serikali yake kuboresha viwanja ambavyo vingi haviko katika hali nzuri.
(Via;TFF)
Post a Comment