FREEMON MBOWE MBARONI KWA TUHUMA ZA KIGAIDI
Leo Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi kuhusiana na
kushikiliwa na Polisi Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowebkutokana na kuwepo na upotoshaji mkubwa kuwa anashikiliwa kwasababu ya kupanga na kuandaa Kongamano la Katiba mpya huko Mwanza.
Kulingana na Jeshi la polisi, limesema Freeman Mbowe alikua anafahamu fika kuwa ana tuhuma
zinazomkabili zinachunguzwa na kwamba wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua nyingine za kisheria mara tu uchunguzi dhidi yake utakapo kamilika hatua ambayo imefikiwa kwa sasa.
Jeshi la polisi limefafanua kuwa, kama ilivyokua kwa baadhi ya watu kucheza na nyakati na matukio akaona ni vyema akimbilie Mwanza kwa kigezo cha Kongamano la Katiba mpya ili akikamatwa umma uamini amekamatwa kwasababu hiyo na kwa bahati mbaya taarifa zilizoenea ndani na nje ya Tanzania kwamba amekamatwa kwasababu ya Kongamano la Katiba mpya.
Aidha, Jeshi la polisi limependa ifahamike kuwa, sasa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
anashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na tuhuma zinazomkabili za kula njama ya kufanya vitendo vya kigaidi ikiwepo kuua viongozi wa
serikali ambapo wenzake sita (6) walishafikishwa Mahakamani.
Jeshi la Polisi limesema linaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutii sheria, kanuni na taratibu za nchi kwa ajili ya kudumisha amani
upendo, mshikamano na utulivu wa nchi yetu.
"Kamwe tusikubali kurubuniwa na baadhi ya watu wanaocheza na nyakati na matukio ili kufanikisha ajenda zao wanazodhani hazifahamiki na wala
hazitajulikana."---- JESHI LA POLISI
Post a Comment