YANGA WAMHOFIA MWAMUZI ALIEPANGWA FAINALI YA ASFC
Uongozi wa klabu ya Yanga SC, umetangaza kushtushwa na chaguo la Mwamuzi Ahmed Arajiga kwa ajili ya kuchezesha mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) utakaofanyika Kigoma, Jumapili ya tarehe 25/07/2021.
Kwa mujibu wa timu hiyo, imesema hali hiyo imetokana na ukweli kwamba Mwamuzi huyo ndiye amehusika katika kuchezesha mechi za wapinzani wao (Simba SC) zilizofutana katika mashindano haya, katika hatua ya Robo Fainali, Nusu fainali na sasa (Simba SC) amepangwa katika Fainali.
Aidha, uongozi wa Yanga umekiri kuwa una amini Tanzania ina waamuzi wengi wenye uwezo, hivyo, kitendo cha kumrudia mwamuzi mmoja katika mechi tatu za timu moja katika shindano moja kinatia shaka kwa Klabu na mashabiki pia
"----->Hivyo basi tunaomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nabMenejimenti ya Mashindano haya kutafakari juu ya uamuzi wa kumtumia mwamuzi huyu katika mchezo huo mkubwa wa Fainali."---- YANGA SC
Post a Comment