PAUL KATEMA ASAJILIWA AZAM FC
Klabu ya Azam FC imeingia mkataba wa miaka miwili na kiungo mkabaji wa kimataifa wa Zambia, Paul Katema, akitokea Red Arrows ya huko.
"Katema ni miongoni mwa viungo bora nchini Zambia, anakuja Azam FC kuongeza nguvu kwenye eneo hilo kuelekea msimu ujao"---- AZAM FC
Huo unakuwa ni usajili wa tano kwa Azam FC, baada ya awali kuwasainisha nyota wengine wawili kutoka Zambia, Charles Zulu, Rodgers Kola, Kenneth Muguna (Kenya) na Edward Manyama (Tanzania).
Post a Comment