POLISI WAMVAMIA MBOWE HOTELINI, WAKAMATA WATU 11

Mratibu wa Uhamasishaji Balaza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA) Bw. Twaha Mwaipaya amesema, polisi wamemvamia Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe.Freeman Mbowe, usiku huu katika Hotel aliyofikia mkoani Mwanza, wakiwa na Gari zaidi ya nne za polisi.

Aidha, amesema polisi wamewakamata watu 11 waliokuwepo kwenye Hotel ya Kingdom hapa Mwanza usiku huu wa manane, sasa Mwenyekiti  Mhe. Freeman Mbowe Alibaki mwenyewe chumbani, na kugoma kufungua mlango wake, na kuwasihi wanachama kuendelea kumuombea.

Licha ya hivyo, Mlango wa chumba alichokuwepo Mhe. Freeman Mbowe hapa Kingdom Hotel Mwanza umevunjwa, Mhe. Mbowe amechukuliwa zaidi ya Dakika 30, lakini hajapelekwa mpaka sasa kuunganishwa na wenzake Central, Polisi wanasema wao hawajamkamata, kwa mujibu wa Twaha Mwaipaya.

Twaha Mwaipaya amethibitisha mpaka sasa waliokamtwa ni;-John Pambalu, John Heche, Rose Mayemba, Benja (kinondoni), Masenya (Mwenyekiti bavich ilemela), Steven Odipo, Prof Rwaitama, Seti (dereva kanda ya victoria), Apollo, Frank Novatus CHASO, na Mwakiaba.

"----->Mpaka muda huu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. FREEMAN MBOWE hajulikani halipo vituo vyote vya Polisi hapa mjini hayupo, tunaendelea kumtafuta, tatizo ni Kongamano la KATIBA MPYA Kesho Mwanza ndio Mteke Mtu saa 8 usiku?"

"----->Pamoja na kwamba Mwenyekiti wetu wa chama Taifa Mhe. Freeman Aikael Mbowe Hajulikani halipo mpaka sasa, na viongozi wengine kukamatwa na Polisi; Kongamano letu lipo palepale"

"Nyamagana na Ilemela Mwanza, tujitokeze kwa wingi tukiwa tumevaa Tisheti zetu za Katiba Mpya."---- TWAHA MWAIPAYA

No comments