EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI

Akati napewa barua ya admision nilifurahi sana ila nikawa nawaza moyoni ntaweza kweli kwasababu moja nikiwaza miundo mbinu ilivyo ya chuo kwanza chuo kikubwa kwa wanaoijua udsm unaweza kupata picha halisi mfano unakipindi yombo 4 kikiisha unatakiwa uwahi kipindi Coet,
Ufike bado unakuta darasa liko juu gorofa ya 4 na hamna lift imagine utafanyaje hapo ndio mgeni hujuani na mtu yoyote yani wala huna mazoea na mtu sasa mimi nilichofanya nikuanzisha mazoea na wanadarasa haraka sana na hii ilinisaidia kutengeneza marafiki na wakajua nini nahitaji kwahio wakawa wananipa kampani kunisukuma kutoka point moja kwenda nyingine kama ni darasani au kwenda canteen nakumbuka nilikuwa nilikuwa na kipindi coet juu gorofa ya 3 hivi au 4 basi wanadarasa wakawa wananinyanyua kutoka chini mpaka juu kipindi kikiisha wananibeba tunashuka hadi chini.

(Nawashukuru sana sana lile darasa) miezi ya mwanzoni kiukweli nilihustle kuna mda ikawa vipindi vingine sihudhurii vya usiku naamua kurudi zangu nyumbani tu ila kesho yake lzm nipate desa nisome na nielekezwe na wenzangu. 

Sasa siku zinavyozidi kwenda nikaanza kuzoea zoea mazingira siku moja nikakutanishwa na kitengo flani hivi kinachodeal na watu wenye changamoto za ulemavu chuoni nikasajiliwa na nikawasilisha mapendekezo yangu nini nahitaji ili maisha yawe mepesi kwangu chuoni.

Tukaanza na swala la vipindi vyote madarasa yawe ni ya chini hili likafanikiwa, pili kutafutwe bajaji mpya kwa ajili ya kutuchukua hostel kutupeleka madarasani na kuturudisha hostel na hata maeneo mengine tukihitaji hili lilifanikiwa japo kwa kuchelewa, njia tunazopita hasa maofisini kuwekwe pavement ili kupita wheelchair hii pia ilifanikiwa lkn pia niliomba lift moja ya jengo la ofisi za wahadhiri wa course yangu itengenezwe hili pia lilifanikiwa. (Naushukuru sana uongozi wa UDSM kwa kipindi kile). 

Pia wakati napewa hostel chumba niliambiwa na dean kuwa naweza kuishi na mtu msaidizi wangu kutoka nyumbani au nitafute mwanafunzi mwenzangu( kiume) ambae atajitolea kuishi na mimi chumba kimoja na kusaidiana ili niwe naishi chuo na kuacha kuwa narudi nyumbani. 

Basi walinipa chumba lkn ilinichukua mda kuhamia.

No comments