AMKA NA BWANA LEO 7

KESHA LA ASUBUHI

IJUMAA, MEI, 7, 2021
SOMO: SIRI YA KUWA NA AFYA NJEMA 

Basi mlapo au mnywapo au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. 

1 Wakorintho 10:31. 



Mungu hahitaji wajumbe Wake wauwasilishe ukweli mzuri wa matengenezo ya afya kwa njia itakayoudhi mioyo ya wengine. Hebu asiwepo mtu atakayeweka kizuizi katika njia ya wale waliopo kwenye giza la ujinga. Wasilisha kanuni za kiasi katika njia ya kuvutia kabisa. Hebu wale wote ambao wanafundisha matengenezo ya afya wajitahidi sana kufanya kile waanacho hubiri kuwa ndivyo kilivyo.... 



Suala la lishe linapaswa kuchunguzwa kwa ustahimilivu. Tunahitaji maarifa na maamuzi ya hekima, ili tuenende kwa hekima katika suala hili. Sheria za asili hazipaswi kupingwa, bali zifuatwe. Afya inapaswa izingatiwe kwa makini. Baadhi ya watu kwa kudhamiria wanaacha kula vyakula visivyofaa, na wakati ule ule wanashindwa kula chakula ambacho kinatoa virutubisho muhimu kwa ajili ya afya ya mwili. Kamwe usitoe ushuhuda dhidi ya matengenezo ya afya kwa kushindwa kupata chakula kikamilifu, chenye ladha kitakachochukua nafasi ya vile vinavyodhuru katika lishe ambavyo tumeviacha. 



Busara nyingi na umakini yapaswa vitumike katika uandaaji wa vyakula ili kuchukua nafasi ya mlo ambao unatumika katika familia nyingi. Kazi hii inahitaji imani, kudhamiria, na jitihada za pamoja, vinginevyo kutakuwa na shida katika suala la matengenezo ya afya. Sisi sote tuna miili ya kufa, na tunapaswa kujiimarisha kwa vyakula vyenye ladha, vyenye afya. Wale ambao hawajui kupika kwa kuzingatia usafi wanapaswa kujifunza namna ya kuchanganya viungo kwa namna ambayo inafanya chakula kuwa chenye ladha nzuri.... 



Hebu tufanye maboresho yenye tija ili kurahisisha mlo wetu. Kwa ukarimu wa Mungu, kila nchi inazalisha vyakula ambavyo vina virutubisho vinavyohitajika kwa ajili ya kuujenga mfumo wa mwili. Vyakula hivi vinaweza kuandaliwa vikawa mlo wenye afya, wenye ladha nzuri. 



Bila kudumu kufanya ubunifu, hakuna atakayeweza kufanikiwa katika mapishi ya afya. Lakini wale wote ambao mioyo yao imefunguka kupokea mafundisho kutoka kwa Mwalimu mkuu watakuwa katika maarifa na ustadi. Watajifunza mambo mengi, pia wataweza kuwafundisha wengine; maana Kristo atawapatia ujuzi na ufahamu. 



—Letter 177, Mei 7, 1901,, kwa ndugu na dada wa Jimbo la Iowa.



No comments