EPSODE 4 NA KANKWI WA KANKWI

Baada ya kuikubali hali yangu na kuona maisha acha yaendelee nikajiuliza kwahio nini kinafuata nikapata wazo la kufungua biashara ili nisikae tu nyumbani lkn pia nipate hela ya mahitaji yangu madogo madogo kila siku, nikawa na idea ya biashara kuuza nguo mtumba za kike grade one, mtaji bahati nzuri chuo nilichokuwa nasoma walinipa nusu ada ambayo kimsingi sikuitumia lkn pia nilikuwa na hela ambayo nilikuwa naiweka mfano akija ndugu au rafiki kunipa pole akinipa hela nikawa natunza. 

Lkn pia nilipata hela kwa kaka mkubwa basi nika tafuta frame maeneo ya nyumbani kimara nikailipia nikaierebisha ikawa sawa nikafuata mzigo nakumbuka ilala sokoni asubuhi sana nilichukua tax hadi huko hii ilikuwa mwaka 2012. 

Nikafanikiwa kupata nguo nikarudi nyumbani nikaziandaa nikaziweka dukani nikaanza biashara hii ilinisaidia kutokukaa tu nyumbani lkn pia kutengeneza network na watu wapita njia na hasa kusocialize. 

Nilifanya hio biashara almost mwaka mzima ndipo nikatamani kurudi tena chuo kusoma maana nilikuwa naona bado elimu yangu haitoshi na niliamini kwa hali yangu hii ili niheshimike Na nitoke kimaisha lazima niwe na vitu flani moja ELIMU kisha PESA itafuata basi nikamshirikisha dada angu then na ndugu baadhi na kuanza kutafuta chuo bahati nzuri ni kapata chuo kikuu UDSM na nikaomba nafasi nikapata mwaka 2013 kusomea SOCIOLOGY. ile biashara niliamua kuifunga ili focus kubwa iwe shule.

Sasa kuna maisha ya chuo baada ya kuanza na changamoto zake na namna nilivyopambana hadi kumaliza haikuwa kitu rahisi kabisa but its very interesting hapa ndipo niliuona Ukuu wa MUNGU na nikaamini zaidi kweli Mungu yupo ukimwita Atakuitikia.

No comments