EPSODE 4 NA KANKWI WA KANKWI

Baada ya kuongelea changamoto hio ya kwanza ya kiafya sasa changamoto nyingine ilikuwa ni ya kimahusiano haha hapa najua wengii mnataka kujua eheee ikawajee kabla na baada ya Ajali nisingependa niongelee sana hii part ila mahusiano yalikuwa kiukweli ni HOVYO wapare wanasema HORRIBLE and TERRIBLE, someone atakuwa hapo just for feeling pity lkn hata kwa upande wangu nilikuwa na makosa kama binadam lkn zaidi hali niliokuwa nikipitia nilikuwa najistukia nahisi kama mda wote nadanganywa japo kuna muda Mungu alikuwa ananionesha ikitokea nadanganywa. 

Binafsi nilipitia mahusiano mengine nilipenda kweli na hata kunigharimu muda na hata pesa na mahusiano mengine hivo hivo tu ilimradi (just triping myself). 

Lakini nawashukuru sana mliowahi kupita katika maisha yangu maana mmenifikisha hapa na Kumpata MKE wangu Jescar Ambae Mungu aliniandalia wa Maisha. 

Asante Jescar kwa Kunipenda.

Changamoto nyingine ya tatu ilikuwa ni uchumi kwa maana kwamba unapokuwa kwenye hali hii matibabu yake ni gharama mno nyinyi wote ni mashahidi lbd unatakiwa uende nje ya nchi na ukiangalia hali ya uchumi wa familia ni mbaya unashindwa najua wapo wenzangu huko hata kwenda tu mazoezi wanashindwa kwasababu ya pesa, wanaohitaji lbd wheelchair wanakosa wanaohitaji lbd dawa na vifaa tiba lkn kwasababu ya pesa wanashindwa, mimi binafsi mpaka leo kuna vitu natamani niwe navyo lkn ndio hivyo ukiangalia gharama zake siziwezi basi unaamua kuji adapt tu hali halisi kikubwa Pumzi.

Basi kwa kumalizia hii episode ya 4 niwaombe wale wote wanaopigania afya zao msichoke iko siku mtatoboa mtaamka hapo kitandani lkn pia niwaombe ndugu zenu na wapendwa wenu msiwachoke wapendeni simameni nao kwa kuwa mnapata thawabu kwa Mungu bila nyinyi kujua. MUNGU awabariki sana

No comments