EPSODE 4 NA KANKWI WA KANKWI

Nikaanza kuikubali hali yangu nikawa nafanya mazoezi kwa nguvu,nakumbuka kuna watu wawili dada aliwaleta hawa watu walikua spesho kwa ajili ya kuchua mwili aisee walikuwa wanachua mwili na dawa zao yani wakimaliza uko hoi ila ilikuwa inasaidia kurudisha uhai wa mishipa ya damu. 

Walikuwa wakinisimamisha huku wanachua nilikuwa mpaka nazimia baada ya dakika kadhaa naamka. 

Basi ikawa huku kuchua huku maombi na mazoezi halafu nikaanza kawakaribisha marafik nyumbani nakumbuka dada alininunulia simu ili nijiunge na Facebook kipindi hiko ndio habari ya mjini nikajiunga nikaanza ku interact na walimwengu ilinisaidia pia nilikutana na ndugu huko na marafiki. 

Mazoezi yakakolea nikatoa mpira wa mkojo nikaanza kujifunza kubana mkojo japo haikuwa rahisi nikaacha kuvaa pampers nikawa nikisikia haja napelekwa chooni..appetite ilirudi kusoma 100%nikauliza je naruhusiwaa nikaambiwa subiri umalize dozi ya sindano.

Kujikubali kukawa ndio nguzo ya mm kuona mabadiliko nikaanza hata kutoka kwenda nje hadi saa nyingine marafiki wanakuja wananichukua tunaenda beach kidogo au hata live band yani basi tu ni interact na walimwengu nijione na mm nipo ilinisaidia sana.ile hali ya kuzimia ikaisha baada ya kupigishwa nyungu za kutosha tena za mavi ya tembo na mazagazaga mengine. 

Nilikuwa nazurura jamani sema hapo bado vidonda havijapona vizuri. 

Nakumbuka hadi kwa Babu wa Loliondo nilifika kutafuta uponyaji wangu. 

Sasa kuna siku nikaenda CCBRT kutafuta daktari wa mazoezi nikakutana na mzungu mmoja alivyonichunguza akaniambia hatuwezi kufanya mazoezi huku una vidonda utaumia na hivi vidonda vitaweza leta infection na vitakuua akanishauri nikulaze kesho asubuhi nikufanyie surgery tuvifunge nikakubali na nikawataarifu ndugu zangu. 

Basi vikafungwa ila sasa nililala miezi 2 kasoro kwa tumbo tu nakula kwa style hio yani ilikuwa ni shidaa sana kwa kweli ila nilipona nikarudi mazoezini.

Na mitikasi mingine ikaendelea furaha ikarudi tena sikumwacha Mungu wangu maisha yalinibadilisha ila ikafika point nikayabadili maisha na kuji adapt na hali halisi kipindi hiki niwashukuru watu wafuatao dada Idda na familia yake,Doris,Anna,Mama na wale wote marafiki zangu hamkunichoka.

No comments