EPSODE 4 NA KANKWI WA KANKWI

Baada ya kurudi Dar kiukweli nilipoteza tumaini sikuona mbele yangu kiufupi nilikata tamaa,japo dada angu na familia yake hawakuchoka waliendelea kunihudumia walipambana huku na kule ili mimi niweze kupona, tulitumia tiba zote unazozijua ww niliombewa na watumishi mbalimbali wenye majina na wasio na majina dini zote nilipita kuombewa. 

Kipindi hiki hata marafiki nilikua nawakwepa wengine kuja kuniona nilikua sijiamini najiuliza sasa akija rafiki yangu yoyote na akiniona na huu mpira wa mkojo au akijua nimevaa pampers itakuaje nilikuwa najisikia vibaya sana, nilikonda mno kwasababu kwanza nilikua sili chakula sina hamu ya kula,maumivu ya vidonda ( bed sores) sindano nilizokuwa nachomwa ( powersafe) mpaka nilikuwa namchukia mchomaji dada angu mmoja hivi ni nurse muhimbili sema kwa sasa namshukuru maana alinipa huduma ya kipekee usiku kuamka kunigeuza nilale ubavu au na mgongo. 

Basi 2008 ikapitaa yote ni kupambana tu unakutana na huyu anakwambia lake ili tu akusaidie basi unaamua kulipokea. 

Kiukweli maneno ya ushauri wa watu yalikuwa ni mengi lkn hayakunisaidia kwasababu moja kubwa SIKUIKUBALI HALI NA NILISHAKATA TAMAA kwahio ikawa ni kama sikio la kufa..sasa 2009 siku hio tu kumekucha nikakutana na ndugu mmoja sikuwa namjua hata alikuja tu akashinda na mimi siku nzima tunaongea tuuu na story za hapa na pale akaongea vitu vingi sana vya kimaisha alikuwa mtumishi nadhani mwanamke kumbe mimi bila kujua alikua kazini ananifanyia( PSS)Pyscho Social Support alikuja kama mara 3 hivi nyumbani asubuhi anaondoka jioni ile session ilinisaidia alinipa munkari wa kuendelea kuishi na nikajiona nina nafasi nyingine Mungu amenipa. 

Ndipo nilipoanza kuikubali hali yangu nikasema kama nikupotea msituni nishapotea kwahio nikubali nimepotea nianze kutafuta namna ya kutoka msituni na nilikumbuka maneno ya Baba sikumoja aliniambia "unatakiwa uamke hapo MAMA ako ndio anakutegemea mtoto wa kiume mimi sitokuwepo duniani mda wote"na nakumbuka alinipa dawa ya kuleta hamu ya kula inaitwa PHAMACTIN hii dawa ilinisaidia sana mpaka leo huwa nawashauri watu watumie hio dawa nilivyokuwa na imani nayo.

No comments