EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI

Baadae nikakutana na vijana wawili hivi dah kama bahati kwangu wao walikuwa wanaishi mabibo hostel nikawaomba kwakuwa tayari walikuwa marafiki zangu kuwa mnaonaje tukiishi wote hostel chuo mkanipa sapoti na huku tukiendelea kusoma pamoja kwakuwa pia tulikuwa darasa moja? 

Walinielewa na tukakubaliana tukae wote (Niwashukuru sana IMMA & NASORO) Mungu awabariki huko mlipo muendelee kuwa na moyo huo huo. Basi nikahamia rasmi chuo na kazi ikawa moja tu kusoma kusoma kusomaa tulikuwa hall 7 chumba namba 103 ground floor haha shule ilipigwa pale kwanza huyo imma ndio CR wetu huyo Nasoro sasa ndio shule ilikuwa ipo hapo mimi binafsi siwezi kujiongelea niliosoma nao watasema wenyewe.

Tuliishi kama mapacha watatu tulipendana sanaa.
Mwaka 2013 ukaishaa sasa ishu ikawa mwaka unaofuata halafu Ada haijulikani itatokea wapi.

No comments