EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI
Basi baada ya mwaka wa kwanza unakaribia kuisha na kufanikiwa kupambana na machangamoto yote kama nilivyoeleza ya mazingira lkn pia hata upande wa ada tulipambana na ndugu kwa kuunga unga ikatimia nikasoma sasa mwaka wa pili unakuja nikawa nawaza sana ada itakuaje nakumbuka nili apply mkopo serikalini na niliamini ningepata tangu first year kwasababu nilikuwa na vigezo vyote mzazi mmoja hayupo mama ni wa nyumbani hakuwa na uwezo haya hali ya ulemavu pia lkn nilitoswa basi nikaanza kupata wasiwasi nikiangalia kwa ndugu nako mtihani mambo yalikuwa magumu nikawaza au nihairishe chuo ili siku nikipata hela nirudi kusoma?!niliwaza mno mno ndipo nikakumbuka yupo Mungu cha kufanya nianze kufunga na kusali kwa ajili ya hio ada ya mwakani ndipo nikanza kusali na kufunga haswa kwa imani nakumbuka nilipungua sana mpaka narudi nyumbani likizo nimeisha hapo UE nazo zilichangia basi nikawa nipo kwenye maombi ya kufunga basi tunakaribia kufungua chuo dada yangu Idda akaniambia mdogo wangu nina pesa kidogo kalipe hiki then tutajua mbeleni basi nikafanya hivo nikarudi lkn bado nina mashaka wasije kunigomea chuo, nikarudi nikalipa hiko kiasi nikaendelea na masomo huku bado nafunga na kusali sasa kuna siku moja nimetoka kanisani misa ya asubuhi jumapili nimekaa sehem nje ya darasa namsubiri Nasoro aje anikokote nirudi hostel kwangu kupumzika ndipo akatokea mama mmoja hivi akanishika bega na kuniambia MWANANGU HUJAMBO nikageuka kuangalia ni nani nikamjibu sijambo mama shikamoo akajibu marahaba akaniuliza mbona uko hapa unamsubiri nani nikamjibu mwenzangu anakuja kunifuata akasema sawa akauliza we ni mwanafunzi nikamjibu ndio akasema nakuonaga kila jpili nikahisi ni ndugu wa staff hapa chuo nikamjibu hapana,akasema basi kila jpili nikikuona natamani kukusalimu roho wa Mungu ananiambia kaongee na yule kijana lkn nashindwa ila leo nimeweza!nikatabasam kidogo nikamwambia sawa mama karibu akaniomba namba yangu ya simu akaniambia kesho nikitoka darasani mchana atanitafuta nikamjibu sawa mama basi akaondoka na mimi nikaondoka nikarudi hostel kupumzika.
Kesho yake nakumbuka saa saba simu yangu ilikuwa inaita nilikuwa nakumbuka nimekaa nje ya chumba changu.
Post a Comment