EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI

Kwanza nimtambulishe kwenu dada Idda au Upendo ndio majina yake Idda Masha.

Tuendelee..basi siku hio nimekaa nje simu ikapigwa ilikuwa jmatatu mchana nikapokea alikuwa ni yule mama nikamsalimia pale akanijibu basi maongezi yakaendelea kwanza akaniuliza mwanangu upo mwaka wa ngapi nikamjibu wa pili,wazazi wako wako wapi nikamjibu mama yupo upareni ila baba alishafariki,ulipata shida gani mpaka ukawa kwenye hiko kiti nikamjibu nilipata ajali ya gari mwaka 2007 akaniambia pole sana nikamjibu asante mama, akaniambia sasa mwanangu mimi Roho wa Mungu mda mrefu alitaka niongee na wewe na nikusaidie ila nikawa kila nikikuona kanisani nashindwa hivo jana niliweza kwa kuwa roho mtakatifu alinipa hio nguvu sasa mwanangu hapo chuo unachangamoto gani ambayo unaipitia ili nikusaidie ? dah nilishusha pumzi na nikamuliza mama upo serious ? Akanijibu ndio wewe niambie nini unahitaji kwa sasa ili nikusaidie nilijikuta tu machozi yananilengalenga nikamwambia mama subiri nikajisogeza pembeni kidogo nikachukua simu nikamwambia mama changamoto ni nyingi sana napitia ila huwezi amini nina mda mrefu nafunga na kusali kwa ajili ya kupata ada ya chuo nimelipa kidogo hata ya nusu semister haijafika kwahio naomba nisaidie ada ya chuo,akanijibu usijali ada yako ni sh ngapi kwa mwaka nikamjibu ni kiasi kadhaa akaniambia basi sawa ntakupa unajua sikuamini akaniambia nipe namba yako inayopokea pesa nikampa akaniambia basi subiri kama masaa 2 hivi nikawa bado siamini akakata simu, mimi nikarudi room huku nafurahi wenzangu wakaanza kuniambia oyaa vipi mbona hatukusomi nikawaadithia wakafurahi. 

Basi baada ya masaa hayo mawili ikaingia hela sikuamini nikampigia simu mama kumshukuru akasema mwanangu kalipe hio ada iliobakia ya nusu semester halafu inayobaki ni pocket money yako dah nilifurahi na kumshukuru sana basi kesho asubuhi tukaenda bank tukalipa Amani ikarudi moyoni mwangu Aisee nikaamini Mungu yupo na aliyasikia maombi yangu. 

Nikampigia simu mama nikamwambia nimeshalipa risiti ntakuonesha jpili akanijibu kuwa na amani ntakuja alhamisi kukusalimia hapo chuoni nikamjibu karibu sana mama angu. 

Ilipofika alhamisi akaja kwanza ujio wake.

No comments