EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI
Basi yule mama alikuja alhamisi kama aliniahidi alipofika hall 7 parking ya magari akanipigia simu akauliza upo wapi mwanangu nikamjibu nakuja kukuchukua basi buana yule mama amekuja na hizi gari za serikali anaendeshwa huwezi mdhania ukimwangalia akashuka kwenye VX moja matata nikampokea akaja mpaka room akapaona kisha akaniambia tukae nje hapa kwenye upepo tukampa kiti tukaanza kuongea kwanza nikamshukuru tena akanijibu kuwa na amani kisha akaniambia yy ni nani,"mwanangu mimi Mungu amenibariki sana na huwa natoa sadaka kwa Mungu kwa kusaidia watu wenye shida mbalimbali hivo Mungu alinionesha ww na akamtuma roho mtakatifu nije niongee na ww na ukaniambia hitaji lako,Wewe ni mwanangu wa 5 kati wale ninaowasaidia" nikamwambia asante sana maana nilikuwa katika kipindi kigumu sana akaniambia kuwa na amani akaniambia subiri kidogo akaenda kwenye gari akarudi na mfuko hivi akaniambia hii ni zawadi yako nikamuliza naweza kuangalia akanijibu sawa nilivyofungua ndani nikaona laptop ndogo ya samsung pamoja na mafuta ya Tb Joshua na stika zake akaniambia najua chuo laptop ni muhimu na hizo stika bandika chumbani kwako na haya maji uwe unajipuliza ukiwa unatoka ukiwa unasoma na hata ukitaka kulala.
Nikamshukuru sana sana sanaaa basi akaniambia naondoka tutaonana jumapili kanisani akafungua pochi yake akanipa pesa kama laki moja nikamwambia mama nina ile balance iliobaki akajibu ongezea kwa ajili ya pocket money pia akaniambia uwaambie ndugu zako na mama pia nikamjibu sawa.
Basi akaondoka ilipofika jioni nikampigia Idda alifurahi na kushukuru nikampigia mama nae akashukuru na kuniambia nimpe namba za huyo mama ampigie amwambie asante nae akafanya hivo. Maisha yakaendelea nikawa nasoma huku nina amani sana yule mama ilikuwaa kila mwisho wa mwezi ananitumia elf 50.
Mungu yupo nyie ukiwa umekwama ukasali na kufunga kwa imani anajibu.
Namshukuru sana Mama Lyimo huko aliko na Mungu ambariki sana.
Sasa ujue Mungu ni mwema siku moja niko zangu darasani simu ikawa inaita nikaipokea kulikuwa hakuna mwalimu nikasikia hallo naongea na david nikamjibu ndio nani ww nikauliza akajibu mimi mtu flani alikuwa ni mdada.
Post a Comment