EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI
Simu ikaita nikapokea alikua ni mdada akaniuliza naongea na Dav nikamjibu ndio uko wapi nikamjibu darasani akauliza mnatoka saa ngapi nikamjibu saa 10 jioni akajibu sawa naomba ukitoka naomba nibeep nikajibu sawa,basi tulivyotoka saa kumi darasani tukaamua leo tusipande bajaji twende mdogo mdogo hadi room kulikuwa mbali kidogo tulifanya hivo kwasababu hio siku ilikuwa ijumaa na hatukuwa na kipindi kingine basi nikambeep yule dada akanipigia akaniambia niko hapa hall 7 nakusubiri nikamjibu sawa.
Tulivyokuwa tunakaribia hall 7 nikaona mtu mbele yetu anachukua video kwa kamera hizi kubwa nikamuliza nasoro na Imma kuna mtu anatuchukua video mnamuona? Wakajibu ndio tusimame tukasimama basi yule dada alinigundua akaniita nikamwitikia wana chuo wengine walihisi kuna movie ya kibongo inachezwa sababu zile kamera zilikuwa zaidi ya moja basi yule dada akaniomba tuendelee kuja tu hamna shida basi tukapanda mpaka kufika parking ya hall 7 yule dada na timu yake wakatusalimia na nikawauliza nini kinaendelea akasema twende room kwako tukaongee nikamkaribisha tulipofika kwanza akauliza mmekula tukamjibu hapana akasema agizeni chakula tukaagiza ndio mazungumzo yakaanza akajitambulisha"Mimi nipo Germany nimekuja kufanya research yangu Tanzania ya PHD ya mazingira na miundombinu ya watu wenye ulemavu vyuoni Tanzania nzima hivo nilivyofika hapa nikapewa namba yako nikaambiwa ww unaweza nipa info vizuri "nikamjibuu ooh karibu sana basi akaandaa kamera zake na kuanza kunifanyia interview,tukaimaliza kisha tukatoka nje na kwenda baadhi ya madarasa na kuona namna inavyokuwa ninavyokaa huku wakichukua video,tukamaliza tukarudi hostel kisha tukaanza stories za kawaida katika stori stori akaniuliza hivi umepata mkopo wa serikali nikamjibu hapana akastuka sana yule dada akauliza kwanini hujapata uliapply nikamjibu nili apply na sijajua mpaka leo kwann sijapata licha ya kufatilia sana. Akaniuliza una baki ya documents zako nikamjibu ndio nikampa akaziangalia akasema una haki ya kupata mkopo nikamwambia ndio hivo sijapewa. Akauliza kesho una ratiba gani nikamjibu kesho ni jmosi nipo tu akaniambia asubuhi nakuja twende bodi ya mikopo, Mungu Huyu.
Post a Comment