DKT, ABBASI AMPONGEZA SALLAM SK

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amempongeza Mkurugenzi wa kituo cha DIZZIM TV, Sallam Ahmed Sharaff (Sallam Sk) kwa uwekezaji alioufanya katika tasnia ya Habari ambao umesaidia kutoa ajira kwa vijana.

Dkt.Abbasi ametoa pongezi hizo leo Julai 9, 2021 Jijini Dar es Salaam wakati akizindua kipindi kipya cha Dizzim Morning kitakachokuwa kinaruka kupitia DIZZIM Tv.


No comments