CHETI CHA DAWA KILICHOBORESHWA KUANZA KUTUMIKA JULAI 10


Wataalamu wa afya wakiwemo waandishi wa dawa (Prescribers) na watoa dawa (Dispenser) katika vituo vyote vya umma ngazi zote za kutolea huduma za afya nchini wametakiwa kuandika na kutoa dawa kwa kutumia cheti cha dawa (Prescription) iliyoboresha kuanzia tarehe 10 Julai, 2021.

Rai hiyo imetolewa leo na Mfamasia Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Daudi Msasi wakati akitoa tamko la matumizi ya cheti cha dawa (Prescription) kwa ngazi zote za kutolea huduma za afya nchini kwenye ukumbi wa Bohari ya Dawa (MSD) jijini Dar es Salaam.

Bw. Msasi amesema kuwa cheti hicho cha dawa itawezesha kuwa na kumbukumbu sahihi za matumizi ya dawa na pia kurahisisha ufuatiliaji wake na kupata ushahidi na katika maboresho ya kitabu hicho waliyofanya wametengeneza nakala tatu ili kuweza kusaidia kulinganisha kilichoandikwa na mtaalam,aliyetoa dawa au mtumiaji aliyepewa bidhaa za afya hivyo siku wakitaka kuhakiki iwe rahisi.

“kutokana na umuhimu wa kufahamu watumiaji wa bidhaa za afya na uwezekano wa kupata ushahidi kutoka kwao juu ya dawa walizopewa, wizara imefanya maboresho kwenye cheti cha daktari kwa kuongeza baadhi ya taarifa ikiwepo namba ya simu ya mgonjwa aliyepewa dawa, jina na cheo cha mtoaji dawa na pia kuanisha kama dawa zilitolewa bure (msamaha) au zililipiwa au zitalipwa na Bima ya Afya”. Alisisitiza Bw. Msasi.

Aliongeza kuwa tayari Bohari ya Dawa (MSD) imeshachapisha vitabu vipatavyo 65,000,000 na ameelekeza MSD kuanza kusambaza na kufikisha kwenye kanda zao nchi nzima ili vituo vya afya waanze kuvitumia na pale wanapoishiwa wanatakiwa kupakua kwenye tovuti ya kwani Wizara tayari imeshakipakia cheti hicho.

Amesema kufuatia kaguzi za dawa zilizofanywa na Wizara ya Afya katika ngazi za Hospitali za Halmashauri na za Rufaa za Mikoa, kulibainika upungufu katika maeneo zaidi ya kumi na sita yenye kuashiria usimamizi hafifu wa bidhaa za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

“Sehemu kubwa ya upungufu huo ni kutotumia ipasavyo miongozo na nyezo muhimu katika utunzaji na utoaji wa bidhaa za afya nchini zilizoa

No comments