BOT KUKAMILISHA AGIZO LA SAMIA KUPUNGUZA RIBA ZA MIKOPO

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kukamilisha haraka maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuhusu taasisi za fedha nchini kupunguza riba za mikopo.

Mhandisi Masauni ametoa agizo hilo Jijini Dar es Salaam alipotembelea Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuzungumza na menejimenti ya benki hiyo.

"Niwapongeze kwa juhudi zilizoanza kuchukuliwa kuwezesha riba kupungua na ikiwezekana mwishoni mwa mwezi huu wananchi waanze kuona matokeo ya juhudi hizo, kwa kuwa kupungua kwa riba ni jambo linalowezekana," ameeleza Mhandisi Masauni.

Pia, ameitaka Benki hiyo kuhakikisha inaweka mikakati mahususi ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni, kwa kuwa na mbinu za kibunifu zikiwemo kuanza kununua na kuhifadhi dhahabu, kuongeza uuzaji wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi na kusimamia kikamilifu shughuli za utalii.

Naibu Gavana Dk. Bernard Kibese, akizungumza katika ziara hiyo ya Naibu waziri Massauni, amesema BoT itaanza kununua na kuhifadhi dhahabu baada ya Kiwanda cha kuchakata madini hayo, kupata hati ya uthibitisho ya uzalishaji wa

No comments