BILIONI 14 KUBORESHA BARABARA KIGOMA VIJIJINI

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, imejipanga kuto shilingi bilioni 14 kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuboresha barabara za vijijini katika Mkoa wa Kigoma.

Hayo yamesemwa Jana Julai 7, 2021 na Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi (OR-TAMISEMI) akizungumza na Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma katika ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo katika maeneo ya elimu msingi na sekondani, huduma za afya msingi, miundombinu ya barabara na ukusanyaji mapato ya ndani.

Mheshimiwa Ummy alieleza kuwa Mheshimiwa Rais Samia Sululu Hassan ametambua changamoto za miundombinu ya barabara hasa katika maeneo ya vijijini, na kuamua kutoa kipaumbele katika kufanya maboresho makubwa sana.

“Salamu za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kwamba anakwenda kutatua kero za miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Kigoma hususan kwa maeneo ya vijijini. Kwa hiyo bajeti ya miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Kigoma inakwenda kupanda kutoka shilingi bilioni 1.2 mpaka shilingi bilioni 14 kwa mwaka,” alisema Mheshimiwa Ummy.

Alieleza kuwa awali kila jimbo katika Mkoa wa Kigoma lilipewa shilingi milioni 500 ambapo kwa sasa zitaongezwa tena shilingi milioni 500 kwa kila jimbo na kupelekea kila jimbo katika Mkoa wa Kigoma kupata jumla ya shilingi bilioni moja kwa mwaka mmoja kwa ajili ya miundombinu ya barabara.

Mheshimiwa Ummy alifafanua kuwa fedha hizi ni tofauti na fedha zinazotolewa kila mwaka kwa ajili ya matengenezo kupitia mfuko wa barabara.

“Kuonesha wanakigoma kazi kubwa amabayo Mheshimiwa Rais anakwenda kuifanya, ni kwamba mkoa mzima wa kigomba ulikuwa una bajeti kwa ajili ya barabara shilingi bilioni moja nukta mbili (1.2 billion) na sasa inakwenda kupanda mpaka shilingi bilioni 14, hongera sana kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,” alisema Ummy.

Aidha Mheshimiwa Ummy alitoa agizo kwa TARURA washirikiane na Madiwani katika utekelezaji wa uboreshaji wa barabara hizo amazo nyingine zitaboreshwa kutoka.

No comments