AMKA NA BWANA LEO 9

*Ijumaa, Julai 09, 2021*

*_Kesha la Asubuhi, Lesoni na Usomaji wa Biblia kwa Mpango_*

```KESHA LA ASUBUHI

Ijumaa, Julai 09, 2021

SOMO: MHIMILI DHIDI YA ADUI```

_*Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa Bwana, na nguzo mpakani mwake kwa Bwana. Isaya 19:19*_

_Mungu anataka kila mtu aelewe wajibu wake wa kutii wito huo, akifanya kazi katika njia ya Bwana, sio kwa kufuata mpango wake mwenyewe. Mungu siku zote hutoa thawabu kwa imani ya watu wake. Njia ya kuelekea katika kiti cha enzi cha rehema iko wazi siku zote. Mungu huona mahitaji ya watu wake katika giza la usiku wa manane kwa uwazi kama vile katika uangavu wa adhuhuri. Kumtafuta Mungu kwa ajili ya msaada wakati wote, huu ndio usalama wetu._

*Mungu anapotupatia ulinzi wake, na kusema juu yetu, "Ninyi ni wafanya kazi pamoja nami," ukidumu katika njia ya Bwana uko salama katikati ya hatari kubwa. Shetani anapotaka kumdanganya mtoto wa imani na tumaini, Mungu huinua bendera dhidi ya adui kwa niaba ya wale wanaofanya kazi kwa makini pamoja naye. Bendera anayoiinua ni sheria yake. Wale wanaotenda haki wana Rafiki wa daima wa kuwasaidia. Katika kila wakati wa shida na mafadhaiko yuko karibu nao. Wanapojaribiwa anajionesha kama mtetezi wao, akisema, "Nitakushauri, jicho langu likikutazama. Nitakusitiri na fitina za watu, na kukuficha katika hema na mashindano ya ndimi."*

*_Bwana haoni kama mwanadamu aonavyo. Wale ambao anawapenda na kuwaheshimu upeo mara nyingi huwa ni malengo ya kejeli na dharau za adui. Anatamani tujifunze somo kwamba hatutapata mafanikio katika kazi hiyo kwa kufuata kigezo cha ulimwengu au mbinu za wanadamu...._*

_Unafiki na kujifanya haviwezi kupata nafasi kwa Mungu. Yote ambayo kwayo tunaweka mikono yetu hutekelezwa [kama vile tuko] mbele ya viumbe vya mbinguni. Mawazo yote ya akili, matamanio yote ya roho, husomwa na Yeye ambaye tunapaswa kutenda pamoja naye. Ushindi unaopatikana na roho haupimwi kwa mwonekano wa nje au kwa sifa za wanadamu, bali kwa wema na rehema na huruma na uaminifu thabiti kwa sheria ya Mungu...._

*_Watu wa Mungu wako katika hatari, ya kufuata desturi za ulimwengu, bila kujali nuru kubwa inayoangaza juu ya njia yao.... Hebu na tudhihirishe tabia zetu halisi. Hebu na tuiinue bendera ambayo juu yake imeandikwa, "Amri za Mungu na imani ya Yesu."_*

```LESONI, JULAI 9

JIFUNZE ZAIDI:

"Walionekana sasa kutubia kwa dhati mwenendo wao dhambi; lakini walihuzunika kwa sababu ya matokeo ya mwelekeo wao mwovu badala ya kutokana na uelewa wa kukosa kwao shukrani na kutotii. Walipogundua Bwana hakuwa na huruma katika hukumu yake, mapenzi yao binafsi yakainuka tena, nao walitangaza kwamba wasingerudi jangwani. Katika kuwaamuru waondoke katika nchi ya adui zao, Mungu alijaribu utii wao wa wazi na kuthibitisha kwamba haukuwa halisi. 

.... Walijua kwamba walitenda dhambi sana kwa kuruhusu hisia zao za haraka kuwatawala na katika kutafuta kuwaua wapelelezi waliowasihi sana wamtii Mungu; bali waliogopeshwa tu kugundua kwamba walifanya kosa la kutisha, matokeo ambayo yangeleta maafa kwao wenyewe. Mioyo yao haikubadilika, nao walitaka tu udhuru ili kufanya maasi yale yale. Hili lilijitokeza wakati Musa, kwa mamlaka ya Mungu, alipowaamuru kurudi jangwani.” —Ellen White, Patriarchs and Prophets, uk. 391.

“Lakini imani haihusiani na majivuno kwa namna yoyote. Ni yeye tu aliye na imani ya kweli ndiye yupo salama dhidi ya majivuno. Maana majivuno ni imani bandia ya Shetani. Imani inadai ahadi za Mungu, na kuzaa matunda katika utii. Majivuno pia hudai ahadi, lakini huzitumia kama Shetani alivyozitumia, ili kupata kisingizio cha kuasi. Imani ingewaongoza wazazi wetu wa kwanza kuutumainia upendo wa Mungu, na kutii amri zake. Majivuno yaliwaongoza kuasi sheria Yake, wakiamini kwamba upendo wake mkuu ungewaokoa dhidi ya madhara ya dhambi. Si imani inayodai neema ya Mbingu bila kufuata masharti ambayo kwayo rehema hutolewa. Imani halisi misingi yake ipo katika ahadi na maelekezo ya Maandiko Matakatifu.”—Ellen G. White, The Desire of Ages, uk. 126.

SWALI LA KUJADILI:

✍️1. Jadili tofauti kati ya imani na Majivuno. Kwa nini kuitwaa nchi ya Kanaani kwanza kulionekana kama tendo la imani na kisha baadaye, Waisraeli walipovamia, inaonekana kama tendo la kujivuna? Ni kwa namna gani kusudi na mazingira vina umuhimu katika utofauti kati ya imani na majivuno? 

¶Tafakari juu ya ukweli kwamba japo dhambi inaweza kusamehewa, mara zote tunaishi na matokeo ya dhambi hizo. Unawezaje kuwasaidia wale wanaopambana na kujua kwamba wamesamehewa dhambi ambayo, hata hivyo, bado inawaathiri kwa njia hasi na, huenda, hata wapendwa wao.

Usomaji wa Biblia Kwa Mpango

YOHANA 3


1. Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.

2. Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.

3. Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

4. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5. Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

6. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

7. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.

8. Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.

9. Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya?

10. Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?

11. Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo twalinena, na lile tuliloliona twalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali.

12. Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?

13. Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.

14. Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

15. ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.

16. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

17. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

18. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

19. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

20. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.

21. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.

22. Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza.

23. Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.

24. Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani.

25. Basi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja juu ya utakaso.

26. Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea.

27. Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.

28. Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake.

29. Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.

30. Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.

31. Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote.

32. Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake.

33. Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli.

34. Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.

35. Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.

36. Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

MUNGU AKUBARIKI SANA```

No comments