ALIYEPOTEA MIAKA 47 ILIYOPITA ARUDI NYUMBANI TENA
Mzee Mwaura, mwenye umri wa miaka 70 nchini Kenya, alitoweka nyumbani miaka 47 iliyopita lakini sasa amerudi, kwa sababu ya media bomba kabisa ya kijamii ambayo ni Facebook, ambayo imemsaidia yeye kuonana na ndugu mtandaoni na kufanikisha kurudi nyumbani.
Mwaura alipotea akiwa na umri wa miaka 23 tu mnamo 1974 baada ya kupelekwa dukani kununua mchele wa familia.
Aliripotiwa kupoteza njia wakati wa mchakato huo, alijikuta akiwa Nairobi hana pesa na hana jamaa wa kumgeukia kwani aligundua kuwa kaka zake ambao walikaa jijini pia walikuwa wamehama.
Kisha akapanda safari kwenda Naro Moru katika Kaunti ya Nyeri ambapo alianza maisha mapya na baadaye akafunga ndoa na mwanamke ambaye alikutana naye huko.
Mwaura, ambaye alifika nyumbani akiwa na suti ya samawati (KATIKATI) aliwajulisha wanafamilia kwamba sasa ameoa na amejaaliwa na ana watoto wanne.
Post a Comment