AMKA NA BWANA LEO 23

*KESHA LA ASUBUHI.*

Ijumaa, 23/07/2021.

*JE, UNAMJUA BWANA WAKO.*

*Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. 1 Yohana 5:10-12.*

▶️Wakati ambapo kwa namna moja tunamjua Kristo, kwamba Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu, inamaanisha zaidi ya hili. Lazima tuwe na maarifa na uzoefu binafsi katika Kristo Yesu, maarifa ya uzoefu na Kristo, kile ambacho Yeye anamaanisha kwetu, na kile ambacho sisi tunamaanisha kwa Kristo. Huo ndio uzoefu ambao unatakiwa kwa kila mtu. Sasa, siwezi kuwa na huo kwa ajili ya yeyote kati yenu, wala hamuwezi kuwa nao kwa ajili yangu. Kazi ambayo inapaswa kufanywa kwetu, inabidi ipitie udhihirisho wa Roho Mtakatifu wa Mungu juu ya akili na mioyo ya wanadamu. Moyo lazima usafishwe na utakaswe.

▶️Sihitajiki kumwambia yeyote kati yenu kwamba ni hivyo, kwa sababu mnaijua. Hakuna hata mmoja wetu anatakiwa kuhisi shaka hata kidogo juu ya mahali tulipo, au kufikiria, "Laiti ningejua mahali niliposimama mbele za Mungu, bali, kwa imani hai, lazima tuzame kwa Mungu; na tutakapofanya hivyo, maisha yake yataangaza juu yetu. Hakuna chembe ya hitaji la sisi kuwa katika hali ya kukosa ufanisi na ubaridi. Tuna shida gani? "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa." Atapewa. Hakuna "ikiwa" au "pamoja na" kuhusu hilo. " Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote" (Yakobo 1:5,6)

▶️Unaomba na kumsihi Mungu kwa ajili ya hekima, nguvu, na ufanisi, na kuhisi kuwa lazima uvipate. Lakini huenda, mara tu baada ya ombi hilo, itaonekana kana kwamba kivuli kibaya mno cha Shetani kimetupwa kinyume na njia yako, na huoni chochote ng'ambo yake. Hiyo ilikuwa nini? Kumbe, ibilisi alitaka kuivuruga imani yako.... Lakini hakuna umuhimu kwako kufanya hivyo. Je! Hisia iwe ndio kigezo kwetu, au ni neno la Mungu aliye hai? Je, tuzamishe imani yetu katika wingu-hofu, wasiwasi? Hilo ndilo Shetani anataka tulifanye....

▶️ *Mara kadhaa wingu hilo lilitua juu yangu, lakini nilijua vilevile kwamba Mungu alikuwepo pale.... "Omba kwa imani, pasipo shaka yoyoye." Usiruhusu pendekezo hata moja la Shetani kuingia. Ni kuwa "hakuna kitu kinachotetereka." Maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari" (aya ya 6). Bwana atatenda mambo makubwa kwa ajili yetu iwapo tu tutaonesha tumaini letu Kwake.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE, TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*

No comments