ALALA POLISI USIKU KUCHA AKIDAI HAKI YAKE

Mwanaume wa Meru nchini Kenya, ambaye alilazimika kulala usiku kwenye kituo cha polisi na mwili wa mkewe ambae ni marehemu alifarijiwa na Mahakama kuu kwa kupewa Ksh.1.5 milioni kwa fidia ya ukiukaji wa haki zake za kibinadamu.

Jaji Edward Murithi aliamuru Charles Mwenda alipwe kwa kukiuka haki zake.

Charles Mwenda anayetoka Tigania, Meru alikuwa amesafiri kutoka Malindi Jumatano, Mei 27, akifuatana na wanafamilia kadhaa kumzika mkewe huko Meru.

Kabla ya kusafiri kwenda nyumbani, Mwenda anadai alikuwa amefuata taratibu zote za kupimwa ugonjwa wa #COVID19 na kupatiwa nyaraka zote  kama kithubtisho kuwa amepimwa.

Akiwa na hati zinazohitajika mkononi, Mwenda alivuka vizuizi vya polisi kutoka Malindi hadi alipofika mpaka wa Meru-Tharaka Nithi, ambapo shida ilianzia apo.

Maafisa hao waliamuru kila mtu atoke ndani ya gari na kudai kila mtu isipokuwa mfiwa ambae ni mwenda arudi Malindi.

"--------> Tulikuwa kwenye kizuizi cha mwisho cha polisi katika mpaka wa Meru-Tharaka Nithi mahali paitwapo Keeria, ambapo tulisimamishwa na polisi na kulazimishwa kutoka kwenye gari, kile nilichoona hapo kilikuwa kibaya sana, familia yangu yote na marafiki walilazimishwa kurudi malindi, ”---> MWENDA

Baada ya tukio hilo, Mwenda ambaye alibaki na mwili wa marehemu mkewe aliingizwa kwenye gari la polisi lililokuwa likisubiri.

No comments