WIZARA YA ARDHI YAENDELEA KUADHIMISHA
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kusikiliza changamoto za watumishi wake walioko kwenye mkoa wa Mtwara na kuzipatia ufumbuzi.
Timu ya Wizara ya Ardhi ikioongozwa na Afisa Utumishi wa Wizara Bi. Mwajabu Masimba tarehe 21 Juni 2021 imekutana na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya ardhi unaohusisha Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mtwara pamoja na halmashauri tisa za mkoa huo.
Timu hiyo ya Wizara inahusisha Afisa Mipango Miji kutoka Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi Makao Makuu Bi. Emilie Mwasyoge pamoja na Afisa kutoka Idara ya Upimaji na Ramani Bi. Siri Mrisho.
Halmashauri ambazo timu ya Wizara ilizungumza na watumishi wake ni Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mtwara DC, Nanyamba Mji, Newala Mji, Newala DC, Masasi Mji, Masasi DC, Nanyumbu na Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeamua kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutembelea watumishi wake walioko ofisi za pembezoni ambapo tayari ilishatembelea watumishi walioko ofisi za ardhi mkoa wa Ruvuma.
Wiki ya Utumishi wa Umma imeanza kuadhimishwa tarehe 16 Juni 2021 na kilele chake itakuwa Juni 23, 2021.

Post a Comment