WATENDAJI ARDHI WATAKIWA KUACHA TOFAUTI KAZINI
Watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Ruvuma wametakiwa kushirikiana na kuacha tofauti zao kwenye utendaji kazi ili kuleta ufanisi na tija katika sekta hiyo.
Hayo yamebainishwa tarehe Juni 19, 2021 na Afisa Utumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mwajabu Masimba alipozungumza na watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Ruvuma wakati wa kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma.
Wizara ya Ardhi inaadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza tarehe 16 Juni 2021 na kufikia kilele tarehe 23 juni 2021 kwa kutembelea ofisi zake zilizoko pembezoni ambapo Wizara hiyo inatembelea ofisi zake za mikoa ya Ruvuma na Mtwara.
Alisema watumishi wa sekta ya ardhi hawatakiwi kutofautiana katika utendaji wowote wa kazi hata kama wako kada tofauti kwa kuwa taofauti yoyote itakayojitokeza haitaleta tija kwenye sekta ya ardhi.
Kwa mujibu wa Bi. Masimba, kufanya kazi maeneo ya pembezo si kama wamewatengwa bali ni sehemu ya majukumu na ndiyo maana Wizara ya Ardhi iliamua kupeleka timu ya maafisa wake ili kujua na kuzipatia ufumbuzi changamoto zao.
‘’Tushirikiane kila moja kwa kazi yake na mkumbuke muda mwingi tunautumia ofisini hivyo ushirikiano mtakaoufanya kwenye utendaji kazi na kuondoa tofauti utaifanya wizara kusonga mbele kwa kuwa taswira nzuri ya ofisi inajengwa na watumishi’’ alisema Masimba.
Naye Afisa Mipango Miji kutoka idara ya Maendeleo ya Mkazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maemdeleo ya Makazi Bi. Emmile Mwasoge aliwatia moyo watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Ruvuma kuwa wasikate tamaa kutokana na changamoto zilizopo na kuwataka kuwa wavumilivu.

Post a Comment