WIZARA YA ARDHI KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANANCHI
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kukutana na watumishi wa ofisi zake zilizopo pembezoni kwa lengo la kusikiliza malalamiko na kero za watumishi.
Timu ya Wizara ya Ardhi ikiongozwa na Afisa Utumishi Bi. Mwajabu Masimba iko mkoani Ruvuma kukutana na watumishi wa sekta ya ardhi kwenye ofisi zake za mkoa huo.
Ofisi hizo ni Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Ruvuma pamoja na zile za halmashauri za Nyasa, Mbinga Mji, Mbinga DC, Songea Manispaa, Songea DC, Madaba, Tunduru pamoja na halmashauri ya Namtumbo.
Kauli mbiu ya Wiki ya Utumishi wa Umma ni kujenga afrika tunayoitaka kupitia utamaduni wa uadilifu unaostawisha uongozi wenye maono hata katika mazingira ya mgogoro.

Post a Comment