WATOA HUDUMA WATAKIWA KUWEKA MIPANGO VIZURI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza watoa huduma za Afya nchini zikiwemo Hospitali na Vituo vya Afya kuweka mipango mizuri ya malipo ya matibabu pale mgonjwa anapolazwa na sio kulimbikiza deni na kuzuia maiti mgonjwa anapofariki.

Rais Samia amesema hayo mapema leo wakati akiongea na Wanawake wa Tanzania kupitia mkutano wa Wanawake wa Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

"Hili la watu kudaiwa wakati mtu amefariki wekeni mipango vizuri, moja ya mipango mizuri ni kutoa gharama za matibabu kabla mgonjwa hajafariki na sio kuwaambia ndugu bila kulipa deni la Milioni 3 au ngapi mwili hauzikwi, hii hapana tukaweke mipango vizuri na sio kuzuia maiti". Amesema Rais Samia

No comments