SHULE ZA KISAYANSI KILA MKOA KWA AJILI YA WANAWAKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuanzia mwezi Julai mwaka huu Serikali yake inaanza ujenzi wa Shule za Bweni ambazo zitakua zikifundisha masomo ya Sayanasi kwa wasichana.

Rais Samia amesema Shule hizo zitajengwa katika kila Mkoa wa Tanzania

*“Mwezi Julai mwaka huu tutaanza kujenga shule za Sekondari za Mabweni kwenye kila mkoa kwa ajili ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wanawake.” Amesema Rais Samia.*

Ujenzi wa Shule hizi za Sayansi hasa kwa wanawake ni mkakati maalum wa Serikali anayoiongoza Rais Samia ili kuhakikisha anawasogeza karibu wanawake na ukuaji wa kasi ya teknolojia pamoja na kuendana na mahitaji ya sasa ya Duna.

Ujenzi huo ukikamilika huenda Tanzania ikawa ndiyo nchi ya kwanza Afrika Mashariki kujenga shule maalum za wasichana ili wasome masomo ya Sayansi tu.

No comments