VIONGOZI WA DINI WAPIGA MARUFUKU NENO 'MWENDAZAKE"

Kamati ya amani ya viongozi wa dini nchini imepiga marufuku, John Pombe Magufuli kuitwa "mwendazake". Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Askofu Peter Konki amesema neno "mwendazake" ni matusi makubwa kwa Magufuli na ametaka wanaotumia neno hilo washtakiwe kwani wanahatarisha amani.

Lakini kwa mujibu wa Kamusi kuu ya Kiswahili ya baraza la Kiswahili nchini (BAKITA) toleo no.2 la mwaka 2017, neno mwendazake linamaanisha "mtu aliyekufa hivi karibuni na anaelekea kuzikwa au mipango ya mazishi yake inaendelea." Mwendazake ni kisawe cha neno marehemu ama hayati.

Je unaamini neno mwendazake ni matusi? Je wanaomuita JPM mwendazake washtakiwe kama alivyoshauri Askofu Konki? Je Askofu apuuzwe, au anunuliwe Kamusi ajifunze Kiswahili? Nini maoni yako?

No comments