MAZIWA NI TIBA

🔴KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.

🔴AFYA NA KIASI.

❣️TRH. 14/06/2021.

🎈SOMO: MAZIWA.

Leo tunaangalia namna ya kutengeneza maziwa safi na bora.

Kuna maziwa ya wanyama kama vile ng'ombe, mbuzi nk. Kuna maziwa ya mama. Lakini kuna maziwa ya Maharage ya Soya ambapo ukiyatengeneza vizuri kabisa unaweza kupata maziwa yako na kutumia kwa afya yako.

Ukitengeneza kilo moja ya soya unapata lita 12 za maziwa.

Umuhimu wa maziwa:

Mfano maziwa ya mama; yana vitamini na protini.

Maziwa hupunguza ugonjwa wa moyo. Maziwa na mayai yanakupa lishe kwa ajili ya afya yako. 

Unapotumia protini nyingi huweza kuleta ugonjwa wa moyo. Hivyo unapaswa kuwa na kiasi. Na ni vyema kula mboga kuliko kula vyakula vinavyotokana na wanyama.

Somo litaendelea kesho!

🔴KAYA NA FAMILIA.

🔴TRH. 14/06/2021.

DEVOTHA SHIMBE.

🔴SOMO: VIKWAZO VINAVYOONDOA SHANGWE KATIKA UCHUMBA.

Vikwazo viko vingi vinaweza kuletwa na wewe au wazazi au marafiki.

1. Kukosa maombi kwa Mungu.

Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure. 
Zaburi 127:1

2. Mahari. Wapendwa mahari siyo malipo wala huuzi mtoto wako. Usitumie mahari kama kigezo cha kurudisha pesa ulizotumia.

Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. 
Wafilipi 4:8

3. Ukabila. Hiki nacho ni kikwazo. Sisi tu wamoja katika Kristo epuka hilo jambo halifai kabisa.

4. Miiko. Hili nalo ni tatizo kubwa. Kwa watu wa Mungu miiko haitakiwi. Epuka miiko ikiwa wewe ni mkristo.

5. Uchumba wa siri. Hili nalo ni tatizo kubwa mno. Usifiche uhusiano wenu uweke wazi.

6. Pesa. Usivutiwe na pesa mpendwa siku zikikoma kwa hakika utalia.

Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu.
Mithali 22:1

7. Kuwa na wachumba wengi. Mpendwa marafiki ni wengi lakini mchumba ni mmoja tu. Epuka kuwa na watu wengi ukiwaita wachumba. Acha tabia hiyo siyo njema. Hiyo huonyesha kwamba hujiamini unashusha staha yako 

8. Msukumo-rika. Usifuate ya wengine wanavyofanya simama peke yako.

9. Usijifungie ndani. Yaani (Position yourself) jionyeshe kwa watu usijifiche.

Naye akasema, Unywe, bwana wangu, akafanya haraka, akatua mtungi wake mkononi mwake, akamnywesha. 
Mwanzo 24:18

Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia zako nitawatekea, hata watakapokwisha kunywa. 
Mwanzo 24:19

Akafanya haraka, akamwaga maji ya mtungi wake katika birika, akapiga mbio kisimani ateke, akawatekea ngamia zake wote. 
Mwanzo 24:20

Basi yule mtu akamkazia macho, akanyamaza, ili ajue kwamba Bwana ameifanikisha safari yake ama sivyo. 
Mwanzo 24:21

Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu, 
Mwanzo 24:22

akasema, U binti wa nani wewe? Tafadhali uniambie. Je! Iko nafasi katika nyumba ya baba yako tupate mahali pa kukaa kwa muda? 
Mwanzo 24:23

Usipojiweka wazi utasubiri sana. Utamachi harusi za wengine na kushona sare sana. Hivyo usijifiche.

10. Ugomvi na mivutano ya kila mara. Yaani hamjaoana mnagombana, je mkioana itakuwaje? Hii dalili siyo nzuri kabisa.

11. Uongo. Huu nao si mzuri, uwe mkweli mpendwa uongo haufai.

Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.
Waefeso 4:25

12. Uwazi uliozidi nao ni tatizo. Eleza mambo yako taratibu si kila mtu ni mnunuzi wengine ni wauliza bei tu. Uwe makini.

13. Kukosa uaminifu. Tendo la ndoa kabla ya ndoa. Ni kikwazo pia.

14. Kukosa kielelezo kwa wazazi. Je, anawasemaje ndugu zako au wazazi wako? Uwe makini sana katika jambo hili.

15. Umbali pia inaweza kuwa kikwazo.

16. Maongezi usiku wa manane.

Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Wimbo Ulio Bora 2:7

17. Mtazamo hasi.

18. Uraibu wa kuangalia mambo ya picha za ngono.

🔴NENO KUU.

TRH. 14/06/2021.

MCH. MARK WALWA MALEKANA.
🔴 SOMO: NGUVU YA MAOMBI MAISHANI.

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 
Mathayo 11:28

Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 
Mathayo 11:29

Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; 
1 Timotheo 2:1

kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. 
1 Timotheo 2:2

Maombi ni nini?

Ni kuinua mawazo, akili na moyo wake kwa Mungu akiomba vitu vyema kwa imani akiamini kwamba Mungu anamsikia. Maombi yanaweza kuwa ya sauti au ya kimoyomoyo.

Mgawanyo wa maombi katika kuomba kuna:

1. Kusifu. Kabla ya kuomba unamsifu Mungu kwanza.

2. Kuungama au kutubu. Mtu anaungama dhambi kwa Mungu.

3. Shukrani. Mtu humshukuru Mungu kwa matendo yake makuu.

4. Kudai au kulalama kwa Mungu. Mtu anaomba akidai ahadi za Mungu.

Yesu aliwambia nini wanafunzi wake?

Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; 
Mathayo 7:7

kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. 
Mathayo 7:8

Hapa kuna mambo matatu: kuomba yaani kutaka msaada kwa Mungu, kutafuta maana yake ni kuhangaika ili upate, bisheni nanyi mtafunguliwa(jaribuni fursa nayi mtafanikiwa)

Kuomba kuna msaada gani kwa mwombaji?

Humsaidia kufungua hazina za mbinguni na kuja kwake.

Maombi yanasaidia kukuza na kuimarisha imani kwa Mungu. Imani ya kujiona unaongea na Mungu kama unavyoongea na rafiki yako wa siku zote.

Hutupatia nguvu ya kusimama imara katika mateso na nyakati ngumu. Hivyo mtu wa maombi hatikisiki kamwe.

Watu wa Biblia waliomba pia mfano:

1. YESU ALIOMBA.

Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. 
Mathayo 14:23

Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. 
Luka 6:12

Imetupasa kuomba na siyo kushinda katika muvi, au tamthilia tukiangalia mambo ya ajabu ajabu.

2. Daudi aliomba.

 Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.
Zaburi 55:17

3. Danieli aliomba.

Hata Danielii, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. 
Danieli 6:10

Hakika iko nguvu katika maombi.

Sababu ya maombi kutojibiwa:

1. Kuishi maisha maovu.

Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo. 
Mithali 28:9

Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu. 
Isaya 1:15

Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; 
Isaya 1:16

jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. 
Isaya 1:17

2. Kuomba pasipo imani. Unapomwendea Mungu amini.

Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 
Yakobo 1:6

Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. 
Yakobo 1:7

3. Kuomba nje ya mapenzi ya Mungu.

Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 
1 Yohana 5:14

Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. 
1 Yohana 5:15

4. Kuomba bila kutoa msamaha.

Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. 
Marko 11:24

Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. 
Marko 11:25

Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.] 
Marko 11:26

5. Kuomba kwa namna isivyostahili.

Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 
Mathayo 6:7

Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. 
Mathayo 6:8

Watu wa mataifa waliombaje?

Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza, wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali, utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya. 
1 Wafalme 18:26

Ikawa, wakati wa adhuhuri, Eliya akawafanyia dhihaka, akasema, Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo; labda anazungumza, au ana shughuli, au anasafiri, au labda amelala, sharti aamshwe. 
1 Wafalme 18:27

Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika. 
1 Wafalme 18:28

6. Kuomba miujiza iliyo ndani ya utendaji wako. Mungu hutupatia muujiza kwa mambo yaliyo juu ya uwezo wetu, siyo yaliyo ndani ya uwezo wetu. Mfano huwezi kuomba kufaulu bila kusoma ukisubiri muujiza wa kufaulu! Usome kwa bidii na maarifa nawe utabarikiwa. Fanya sehemu yako na Mungu atafanya sehemu yake.

*MUNGU ATUBARIKI SOTE, IMETUPASA KUOMBA.*

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

No comments