UMMY MWALIMU AFUNGA KIKAO KAZI WAKUU WA IDARA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu wakati akifunga Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma- Chuo cha Mipango Dodoma
1. Kuna haja ya kuiangalia Sheria inayosimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa, sioni afya kwa Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi kuwa Baraza la Madiwani kuna wanaoazimiwa kwa kuonewa kutokana na mazingira hayo katibu Mkuu Utumishi hili tunalileta kwako tuliangalie upya Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi hawa iwe Sekretariet ya Mikoa na Sio Baraza la Madiwani kama ilivyo sasa ‘
2. Maafisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa hamsemwi vizuri mmekuwa Miunguwatu ukikuta Afisa Utumishi wa aina hiyo akaungana na Mkurugenzi wake , Mwekahazina, Afisa Mipango na Mwanasheria basi hapo watumishi wengine wataonewa kila siku mkajirekebishe
3. Katika Hili nitakwenda kuzifumua CMT zote za Halmashauri nasubiria tu Mkeka wa Wakurugenzi utoke, tutazichambua kwa kina kuona ubora wa wajumbe wanaounda hizo CMT na sio wao wanajipendelea tu na kuwasahau wafanyakazi wa chini hili sitalikubali na ntalikomesha
4. Katika Sekretariet za Mikoa katibu Mkuu Utumishi hili pia ntalileta kwako nataka Makatibu Tawala Wasaidizi (Ass) wawe watu watu wenye Uwezo na Weledi Mkubwa wa kuzisimamia na kuzielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa na sio watu wanaowaogopa Wakurugenzi wa Halmashauri na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
5. Maafisa Utumishi mkaangalie namna ya kutoa Motisha kwa watumishi wenu haswa wa zile Kada za chini, motisha sio lazima iwe hela hata Recognition tu inatosha mnaweza kuwapa Vyeti na kuwapongeza kwa kazi nzuri na sio kusubiria kutoa adhabu tu.
6. Katika changamoto ya Uhaba wa Watumishi hivi karibuni tutao Orodha ya Majina ya waliochaguliwa kwa nafasi za Elimu na Kada Mbalimbali za Afya. Uchaguzi umefanyika kwa Haki na umezingatia sifa zao na sio vimemo niwahakikishie kuwa tumezingatia vigezo vilivyowekwa.
7. Na Pia tumezingatia maslahi ya Watumishi na Katika Bajeti ya Serikali Kuu 2021/22 Serikali Imetenga Posho ya Tsh. 100,000 kwa ajili Ajili ya Watendaji Kata wote Nchini na Tsh. 100,000 kwa ajili ya Maafisa Tarafa wote Nchini.

Post a Comment