TIMU 4 KUSHIRIKI CAF

Shirikisho la Soka Nchini Tanzania TFF, limesema kuwa;, Tanzania ni miongoni mwa Nchi 12 zitakazoshirikisha timu nne kwenye mashindano ya CAF 2021/22.

Timu mbili zitacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na Timu mbili nyingine zitacheza Kombe la Shirikisho Afrika.

Hatua ya raundi ya awali itachezwa kati ya Septemba 10-12, 2021 na marudiano kati ya Septemba 17-19, 2021.

Hatua ya makundi itachezwa kati ya Februari 11-13, 2022.

Nafasi hizo zimepatikana baada ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zilizokusanya alama nyingi zaidi kwenye viwango vya CAF.

(Via:@tanfootball)

No comments