ASHAMBULIWA NA FISI

Wafanya upasuaji wa Nchini Afrika Kusini wanatarajia kuunda upya uso wa kijana wa miaka 9 wa Zimbabwe aliyejeruhiwa na fisi katika shambulio lililofanyika mwezi uliopita.

Rodwell Khomazana alipoteza pua yake, jicho la kushoto, mdomo wake ambao ulishambuliwa sana upande wa juu, na sehemu zingine za uso wake wakati aliposhambuliwa akiwa  ibadani usiku mjini Harare.

Madaktari katika moja ya hospitali kuu za umma za jiji hilo walijitahidi kadri wawezavyo ili kuuweka sawa uso wake na kutuliza hali yake, lakini walikosa rasilimali za kurekebisha uso wake ulioharibiwa.

No comments