MUIGIZAJI RAY AMUOMBA RAIS SAMIA KUPUNGUZA KODI

Kutoka kwenye Ukurasa wa Ray ameandika;

Hongera Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan kwa kugeukia Tasnia zinazogusa Michezo na Utamaduni.

Kitendo cha Kutoa Msamaha wa kutotoza Kodi kwenye Nyasi bandia kuvitia Nakshi Viwanja vyetu nicha Kupigiwa Mfano. Kuziagiza Redio kupiga muziki wa Bongoflava maana yake sasa wanamuziki wanakwenda kufaidika na Milahaba.

Mama Samia tukuombe sasa sisi wanao wa Bongo Movie utugeukie pia kwa kuyatazama mambo haya ambayo naamini yataboresha vipatoghafi kwa wasanii wa Sinema.

1. Tunaomba punguzo la Withholding Tax kutoka asilimia 15% hadi 5% maana eneo hili ndilo linalo masikinisha Wasanii wengi.

2. Aidha tunaheshimu kato la VAT kwa asilimia 18,% lakini hapa napo ni eneo ambalo tunaomba basi angalau VAT iwe kws 10% ama 5% Mama ikikupendeza maana ukombozi wa msanii ndio ongezeko la pato kwa waliowengi kwa manufaa ya nchi yetu. @samia_suluhu_hassan

3. Mwisho ni suala la Matangazo ambalo kwa mujibu wa Sheria hayaruhusiwi kwenye paytv. Sisi ambao tunaishi wa Series tukipewa idhini ya kuweka matangazo angalau kidogo basi itatupunguzia ukali wa mapambano ya jasho letu na kukuza kipato kinachochangia ukuaji wa uchumi wetu.

Naamini Mheshimiwa Raisi kupitia Ukurasa huu kwa andiko hili basi utaguswa na maombi haya na kuyatazama kwa JICHO LA ZIADA..-----> @raythegreatest 

No comments