TANESCO KUIMARISHA HUDUMA KWA WATEJA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limejipanga kuimarisha na kuboresha masuala ya huduma kwa wateja ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa Umeme wa uhakika na kutatua changamoto za wateja kwa wakati.

Hayo yamesemwa Juni 6, 2021 na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayesimamia Usambazaji na huduma kwa wateja, Mhandisi Raymond Seya akihitimisha kikao kazi cha Maafisa huduma kwa wateja wa TANESCO Nchi nzima kilichofanyika kwa Siku 7 Jijini Tanga.

Mhandisi Seya ameeleza kuwa, mikakati ya TANESCO ni kuendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa kufanya matengenezo ya Miundombinu kwa wakati sambamba na kuharakisha ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za wateja kwa wakati ili kupunguza malalamiko yanayohusiana na huduma za TANESCO kwa wateja.

No comments