CHANJI; WEKENI MKAKATI UTAKAO ONGEZA UWAJIBIKAJI

Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Usafirishaji Umeme), Mhandisi Isaac Chanji amewaagiza Maafisa Manunuzi na Ugavi TANESCO kutoka na mkakati unaotekelezeka na kuongeza uwajibikaji kwenye maeneo ya kazi.

Mhandisi Chanji amesema hayo leo Juni 07, 2021 wakati akifungua kongamano la pili la Maafisa Manunuzi na Ugavi katika ukumbi wa Rock City Jijini Mwanza.

"Nimejulishwa kuwa kauli mbiu ya kongamano hili ni uwajibikaji katika manunuzi, kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa, niwaombe mkawajibike ikiwa kama ilivyo katika kaulimbiu hii" amesema Mhandisi Chanji.

Aliongeza kuwa, Idara ya manunuzi ni kiungo kinachounganisha Idara zote katika suala la manunuzi, ili kutekeleza majukumu ya Shirika kwa kushirikiana.

Aidha, amewataka kutekeleza Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake pamoja na kanuni, pia Shirika litaendelea kuwapa mafunzo ili kuwajengea uwezo.

No comments