TAASISI ZA AFYA NCHINI ZATAKIWA KUTEKELEZA IPASAVYO


Taasisi zote za afya nchini zimeagizwa kuhakikisha zinatekeleza ipasavyo maelekezo yaliyotolewa na Serikali ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya CORONA vinavyosababisha ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID - 19).

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza itafanya ukaguzi kuangalia iwapo maelekezo hayo yanazingatiwa na Taasisi hizo pamoja na watumishi wake.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Abel Makubi amesema hayo alipozungumza na watumishi wa wizara hiyo kuhusu mambo mbalimbali yatayotekelezwa na Wizara hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika Juni 18, hadi 23, mwaka huu.

"Watumishi wazingatie maelekezo ya kujikinga na CORONA, tumeweza kuudhibiti ugonjwa huu, kuna tishio nchi za jirani ... tuendelee kuchukua tahadhari za Kinga zote.

"Taasisi za afya zihakikishe zinaweka vifaa vya maji safi tiririka na sabuni, wanawe mikono na zile zinazojiweza waweke 'sanitizer'," amesema.

Amesisitiza "Tutakagua baada ya muda, maeneo yenye msongamano vaa barakoa... tumeshaelekeza hili, kwa mfano kwenye mazishi, kanisani, hospitali, daladala na maeneo mengine ambayo ni 'high risk', watu wavae barakoa.

"Au wazingatie umbali unaoruhusiwa zaidi ya mita moja na kuendelea pamoja na kufanya mazoezi kwani yanatusaidia.. si tu kupunguza kupata magonjwa yasiyoambukiza hata haya ya kuambukiza.

Katika kutekeleza maadhimisho ya Wiki hiyo ya Utumishi wa Umma inayoratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Prof. Makubi ametoa rai kwa watumishi wa sekta hiyo kuwajibika,
kuongeza kasi ya utendaji kazi na uadilifu.

"Tuwe wazalendo, tuisimamie sekta hii, sisi ndiyo wa kuibadilisha itoke hapa tulipo, isonge mbele kwa kujituma, nidhamu ya kazi pia tuizingatie zingatei na huduma bora kwa mteja

No comments