KAYA NA FAMILIA LEO 19


*KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.*

*KAYA NA FAMILIA.*

TRH. 19/06/2021.

DEVOTHA SHIMBE.

*SOMO: MAMBO YA PESA KATIKA NDOA.*

Leo tunaendelea na somo letu kama tulivyo angalia jana, kwamba suala la pesa linaweza kufanikisha au kuangusha ndoa endapo zitasimamiwa ndivyo sivyo.

Sababu za migogoro ya pesa katika ndoa:

1. Tofauti za mitazamo katika pesa. Husababishwa na mitazamo potofu na tafsiri mbaya za Biblia. Mfano msisumbukiee ya kesho.... Suluhu ni nini tafuta mafundisho kuhusu pesa.

2. Kukosa uwazi wa matumizi ya pesa. Yaani mtu hutenda kwa siri na mwenzi mwingine hajui. Hivyo hii nayo ni hatari. Wengine wamejenga nyumba bila kutoa taarifa nyumbani akifa tu vinachukuliwa na wengine. Suluhu ya hili panga mambo yenu kwa bajeti yenye mpangilio sahihi hii ni njema kabisa na huleta shangwe.

3. Madeni ya siri. Hii nayo ni changamoto katika ndoa. Epuka madeni uwe mkweli usiwe msiri katika jambo hili. Wengine hukopa kwa kutumia hati za nyumba na wapo kimya hii haifai kabisa. Suluhu: uwazi na ukweli unahitajika.

4. Matumizi mabaya ya nguvu ya pesa. Je, nyumba inaongozwa na upendo au pesa? Mwenye kiasi kingi au cha chini je mnaishije katika hali hiyo? Suluhisho: Mpeandane heshimianeni wote nyie ni mwili mmoja. Pesa haikupeleki popote pale uwe makini.

5. Misaada kwa ndugu, jamaa na marafiki. Mfano mwanamke au mwanaume anatoa msaada kwa upendeleo na usiri. Hivyo hii nayo ni hatari. Toa msaada kwa uwiano sawa na ndani ya kipato chenu. Suluhu: Tumia asilimia ya dharura ya bajeti kuwasaidia ikiwa ni wazazi. Hata hivyo huwezi kutatua matatizo yote ya ndugu, uwe makini katika hili hutayamaliza yote. Familia yako ni ya kwanza.

6. Mabadiliko katika kipato. Kupandishwa au kushushwa cheo, au kupunguziwa mshahara hii nayo ni changamoto. Suluhu: Jenga utaratibu wa kuweka akiba  ili kikabiliana na jambo hili, unganeni kwa pamoja msitengane.

7. Kuishi sehemu tofauti. Hii husababisha gharama kubwa. Safari za mara kwa mara. Hii ni hatari pia. Uvnjifu wa imani kwa mwenzi wako. Suluhu: Chagua kati ya ndoa au kazi, fanya maamuzi magumu. Au jiajiri. Epuka ndoa ya kuishi mkoa huu na mwingine mkoa huu ni hatari sana hii.

Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. 
Mwanzo 2:18

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*

chirongemagai74@gmail.com
🙏🙏🙏🙏

No comments