RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI KWA WENYEVITI WANNE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Juni, 2021 amefanya uteuzi wa Wenyeviti wanne (4) wa Bodi za Wakurugenzi kama ifuatavyo:-
1. Amemteua Dkt. Fenella Ephraim Mukangara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Dkt. Mukangara ni
Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
2. Amemteua Brig. (Mstaafu) Aloyce Damian Mwanjile kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania.
3. Amemteua Bw. Khalfan Ramadhani Khalfan kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
4. Amemteun Capt. Mussa Mandia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 19 Juni, 2021.
Post a Comment