SEKTA YA ELIMU WATAKIWA KUTOA MAONI MABORESHO MITAALA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako (Mb) amewataka wadau wa Sekta ya Elimu kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yatakayosaidia Taifa kuwa na mtaala bora wa kuzingatia ujuzi na maarifa.

Waziri Ndalichako amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau kuhusu maoni ya kuboresha mitaala ya elimu ya awali, msingi na sekondari ili kukidhi mahitaji ya Tanzania ya uchumi wa kati na viwanda.

Amesema Serikali imekuwa ikifanya uboreshaji wa mitaala pindi mzunguko wa elimu unapokamilika au pale ambapo kunakuwa na mahitaji au mabadiliko muhimu katika Nchi, Kanda na Dunia kwa ujumla na kwamba lengo la mabadiliko ya mitaala mara zote limekuwa ni kuhakikisha kuwa mitaala inaendana na hali halisi ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia katika nchi na dunia na kuwa toka nchi ipate uhuru mitaala imeshafanyiwa mabadiliko makubwa mara tano.

No comments