DAWASA YAFIKA MALOLO
MAMLAKA ya Majisafi na usafi wa mazingira Dar es salaam (DAWASA), Mkoa wa Kihuduma Mabwepande, imeongeza mtandao wa upatikanaji wa maji katika eneo hilo ambao lililikuwa halipati maji hususan mtaa wa Malolo Kata ya Bunju.
Ni baada ya kukamilisha mradi ulioanza mwezi huu kwa kulaza bomba lenye ukubwa wa inchi 1.5, umbali wa mita 600 uliogharimu Shilingi milioni 4, fedha za ndani.
Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Juma Kalemera amesema, nia ya kutekeleza mradi huu ni baada ya kuona uhitaji wa wananchi juu ya huduma ya Majisafi ambayo ilikuwa haijafikiwa awali.
“Mradi una lengo la kuongeza mtandao, kusogeza huduma kwa wananchi waliokuwa nje ya mtandao wa DAWASA ili kusaidia kuongeza mauzo ya maji na kuongeza mapato,” amesema Mhandisi Kalemera.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, wamefurahishwa na jitihada za DAWASA za kuwasogezea huduma hiyo ambayo haikuwepo.
Mwanaisha Hamduni amesema, “tunawashukuru DAWASA kutusogezea huduma ya maji katika mtaa wetu, maji tuliyahitaji na sasa tumeyapata, tunaamini shughuli zetu zilizokua zikikwama au kuchelewaa kwajili ya kukosa maji sasa zitakwenda vizuri na maendeleo yataonekana.”
Pia, Mwanaisha amesema, wataokoa muda mwingi waliokuwa wakitumia kutafuta huduma hiyo.
DAWASA inaendelea kufanya jitihada kuhakikisha inawafikia wananchi wote hasa waliopo nje ya mtandao ili kuhakikisha wananufaika na huduma ya Majisafi.

Post a Comment