SABAYA ALIJIPATIA MILIONI 500
January 18 mwaka 2019 aliyekua mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya anadaiwa kujipatia zaidi ya TZS 500M kwa njia za udanganyifu. Sabaya aliwaandikia barua wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa wilayani humo akitaka kila mmoja kuchangia kiasi kisichopungua 15M kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya miezi sita toka ateuliwe.
Jumla ya wawekezaji 35 waliandikiwa barua na kulazimishwa kuchangia sherehe hizo. Wale walioshindwa walipewa usumbufu katika biashara zao ikiwemo madai ya kukwepa kodi. Mmoja wa waliokumbwa na kadhia hiyo ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudley inayomiliki mashamba ya Kibo na Kikafu Estate, Bw.Jensen Natai ambaye aliwekwa rumande kwa siku 3 na kunyang'anywa hati yake ya kusafiria (passport) kwa madai 'feki' ya kukwepa kodi.
Mfanyabiashara mmoja aliyewekeza kituo cha mafuta wilayani Hai ameonesha barua aliyoandikiwa na Sabaya na bank transfer ambayo alituma kiasi cha TZS 15M, ili kugharamia sherehe hizo za miezi 6 ya Sabaya ofisini. Hata hivyo baada ya kukusanaya fedha hizo hakuna sherehe yoyote iliyofanyika, na haijaelezwa fedha hizo zilitumikaje.
Inadaiwa kuwa moja ya mbinu alizokua akizitumia kuwatisha wafanyabiashara ni kujirekodi kila anapoongea na viongozi wakubwa wa serikali akiwemo JPM. Alikua anawasikilizisha wafanyabiashara hao maongezi yake na JPM halafu anawahakikishia kulinda biashara zao kwa sababu yupo karibu na mzee.!

Post a Comment