RAIS SAMIA KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA LISHE DUNI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake itaendelea kulisimamia na kulipa kipaumbele suala la Lishe duni, ikiwa ni Mkakati wa kuhakikisha Nchi inaondokana na tatizo la Utapia Mlo na lishe duni kwa Watanzania.
Rais Samia amesema hayo wakati akiongea na wahariri, waandishi na wataalamu wa Habari nchini jijini Dar es Salaa, kwa lengo lakutathmini hali ya utendandaji kazi wa Serikali yake ndani ya Siku 100.
Akijibu moja ya swali lililoulizwa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bibi Joyce Shebe, aliyetaka kujua makakati wa masuala ya Lishe kwa Watanzania.
Akijibu swali hilo Mhe. Rais alisema, mpango wa kukabiliana na masuala ya Utapia mlo na Lishe duni, alianza akiwa Makamu wa Rais, hivyo kwa nafasi yake kwa sasa, ataendeleza mkakati huo, kwakuwa tayari wakuu wa Mikoa walisha ingia mkataba wa Lishe toka mwaka 2018.
“Kwa sasa nitafanya kazi hiyo nikiwa kwenye kiti hiki cha Urais ambapo najua wakuu wa Mikoa watakwenda kujituma zaidi ili kuondosha tatizo hili, kwani tatizo kubwa tumegundua ni elimu kwa wananchi wetu, lakini wakielimishwa vizuri, wanaelewa” alisema Rais Samia.
Mwezi Desemba, 2018 Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kwa maelekezo ya aliyekuwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, waliingia Mkataba na Wakuu wa Mikoa, kwaniaba ya Makamu wa Rais kwa Mikoa yote Tanzania na kuweka viashiria 11, kama Vigezo vya kutathmini hali ya Lishe nchini huku utekelezaji wake ukianza Mwezi kuanza Januari2019.

Post a Comment