JACOB ZUMA AHUKUMIWA KUFUNGWA MIEZI 15 JELA

Mahakama ya kikatiba ya Afrika Kusini imeamua kuwa Rais wa zamani Jacob Zuma alikuwa akiidharau Mahakama kwa kushindwa kufika kwenye uchunguzi wa ufisadi mapema mwaka huu, na kuamuru afungwe jela kwa miezi 15.

Zuma alishindwa kufika kwenye uchunguzi ulioongozwa na jaji mkuu, Raymond Zondo, mnamo Februari. 

Uchunguzi huo unachunguza madai ya ufisadi wa kiwango cha juu wakati wa kipindi cha Zuma akiwa madarakani kutoka 2009 hadi 2018. 

Anakanusha makosa na hadi sasa hajataka kutoa ushirikiano wowote.

No comments