NENO KUU SIKU YA 18

KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE*

23/06/2021, SIKU YA 18

NENO KUU

Pastor. Mark Walwa Malekana

*_SOMO: MWANAMKE SAFI NI NANI?_*

Mathayo 11:28-29

Mathayo 11:28
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Mathayo 11:29
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

Biblia hutumia mifano mingi ili watu waweze kuelewa haraka na vizuri. Yesu alitumia mifano  kama ya wavuvi, mtumwa, mwana mpotevu n.k ili wanafunzi wake waelewe masomo yake kirahisi.

Mungu anapozungumzia kuhusu Kanisa analifananisha na mlima sayuni, bibi harusi wake n.k

Ufunuo 19:7-8

Ufunuo wa Yohana 19:8
Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

Ufunuo wa Yohana 19:9
Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.

Kanisa ni jumuiya ya watu ambao  Mungu amewaweka na kuwatenga kando kwa ajili ya kuwa watumishi wake.

MUNGU ANALITAMBULISHAJE KANISA LAKE?

Isaya 55:5,6

Isaya 55:5
Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.

Isaya 55:6
Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;

Yeremia 3:14
Yeremia 3:14
Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;

Mungu anajitambulisha kama Mme.

PAULO ALIMPOSEA KRISTO BIKIRA SAFI

2 Wakorintho 11:2
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.

WANAUME WAWAPENDE WAKE ZAO KAMA KRISTO ALIVYOLIPENDA KANISA

Waefeso 5:25,26,27,32
Waefeso 5:25
Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

Waefeso 5:26
ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;

Waefeso 5:27
apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Waefeso 5:28
Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.

Waefeso 5:32
Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa.

KITENDO CHA KUMWACHA MUNGU NI UZINZI

Hosea 1:2; 5:3,4; 6:10; 9:1
Hosea 1:2
Hapo kwanza BWANA aliponena kwa kinywa cha Hosea, BWANA alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha BWANA.

Hosea 5:3
Mimi namjua Efraimu, wala Israeli hakufichwa nisimwone; maana sasa, Ee Efraimu, umefanya uzinzi; Israeli ametiwa unajisi.

Hosea 5:4
Matendo yao hayatawaacha kumgeukia Mungu wao; maana roho ya uzinzi imo ndani yao, wala hawamjui BWANA.

Hosea 6:10
Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo bovu kabisa; huko uzinzi umeonekana katika Efraimu; Israeli ametiwa unajisi.

Hosea 9:1
Usifurahi, Israeli, kwa sababu ya furaha, kama hao mataifa; kwa kuwa umezini juu ya Mungu wako, umependa ujira katika kila sakafu ya nafaka.

MWANAMKE KAHABA NI YULE ALIYEASI NA KUINGIZA MAFUNDISHO YA KIPAGANI

Ufunuo 17:1-5
Ufunuo wa Yohana 17:1
Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;

Ufunuo wa Yohana 17:2
ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.

Ufunuo wa Yohana 17:3
Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.

Ufunuo wa Yohana 17:4
Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

Ufunuo wa Yohana 17:5
Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

Ameketi juu ya maji mengi

Ufunuo wa Yohana 17:15
Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.

MWANAMKE SAFI NI YULE ASHIKAYE MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU

Ufunuo wa Yohana 12:1
Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.

Zaburi 119:105
Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

MAFUNDISHO YAKE YAMEJENGWA 

Waefeso 2:19
Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.

Waefeso 2:20
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.

KANISA HILI SAFI LINAKASIRIKIWA NA JOKA (SHETANI) KWA KUWA LINATII

Ufunuo wa Yohana 12:17
Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.

USHUHUDA WA YESU KRISTO NI NINI?

Ufunuo wa Yohana 19:10
Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.

Isaya 8:20
Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.

HUITWA WATAKATIFU WENYE KUTUNZA AMRI ZA MUNGU

Ufunuo wa Yohana 14:12
Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.

HALIITWI KUWA KANISA LA MUNGU HUKU LIKIWA NA CHAKULA CHAKE CHENYEWE

Isaya 4:1
Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.

Tahadhari aliyoitoa Yesu
Mathayo 7:21-23

Mathayo 7:21
Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

Mathayo 7:22
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

Mathayo 7:23
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Mwisho

Yoshua 24:14-15
Yoshua 24:14
Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA.

Yoshua 24:15
Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.

Kristo anatualika kufuata mapenzi ya Mungu na kutembea katika njia yake.
Tunaokolewa kwa mapenzi ya Mungu sio kwa dini zetu. Tukubali kumfuata Kristo.

TUBARIKIWE SOTE

No comments