AMKA NA BWANA LEO 25
KESHA LA ASUBUHI
IJUMAA, JUNI, 25, 2021
SOMO: MAISHA YENYE AFYA
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
1 Wakorintho 6:19, 20.
Wajumbe wa kwanza wa injili walitumwa pamoja na neno, “Ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 10:7). Huu ndio ujumbe wa leo. Tunapaswa kukumbuka kwamba kazi ya kuzifikia roho haiwezi kufungwa katika njia moja. Umishenari wa injili ya utabibu inapaswa kupelekwa mbele, si kwa mitazamo ya mtu mmoja, bali kwa kumfuata Kristo. Yote yanayofanywa ni kuonesha mvuto wa Roho Mtakatifu. Tunapaswa kufanya kazi kama Kristo alivyofanya kazi. Ndipo tutakuwa salama.
Utume wa Mungu hauhitaji matengenezo. Njia ya Kristo ya kuuwasilisha ukweli haiwezi kurekebishwa. Mfanyakazi ambaye anajaribu kutumia mbinu ambazo zinavutia akili za kidunia, akidhania kwamba njia hii itaondoa vipingamizi ambavyo wanahisi dhidi ya kuuchukua msalaba, anahafifisha mvuto wake. Hifadhi usahili wa utauwa. Baraka ya Bwana haipo kwa mtumishi ambaye hotuba yake ina mhuri wa mambo ya kidunia. Lakini anabariki maneno ya yule ambaye anapenda usahili wa haki ya kweli.
Kazi yetu yapasa iwe ya kivitendo. Tunapaswa kukumbuka kwamba mwanadamu ana mwili vile vile roho kwa ajili ya kuokolewa. Kazi yetu hujumuisha zaidi ya kusimama mbele ya watu na kuwahubiria. Katika kazi yetu tunapaswa kuhudumia udhaifu wa kimwili wa wale ambao tumekutana nao. Tunapaswa kuwasilisha kanuni za matengenezo ya afya, tukiwavutia wasikilizaji wetu kwa mawazo ambayo yana sehemu ya kufanya ili kuwafanya wawe wenye afya.
Mwili unapaswa kuwa wenye hali ya afya ili roho iwe na afya. Hali ya mwili inaathiri hali ya roho. Yeye mwenye uwezo wa kimwili na kiroho anapaswa kuwa na mwelekeo sahihi kuhusu vyakula. Anapaswa kuwa makini asiilemee roho kwa kuchosha nguvu zake za kimwili au za kiroho. Kwa kuzingatia kwa uaminifu kanuni sahihi za kula, kunywa, na kuvaa ni wajibu ambao Mungu ametupatia wanadamu.
Bwana anatamani tutii sheria za afya na uzima. Anamwajibisha kila mtu ili atunze kwa usahihi mwili wake, ili uwe katika afya.
—Barua ya 123, Juni 25, 1903,, kwa Edson na Emma White.
Post a Comment