KAYA NA FAMILIA SIKU YA 18
KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE*
23/06/2021, SIKU YA 18
KAYA NA FAMILIA
Mama DEVOTA SHIMBE
*SOMO: MALEZI YA WATOTO*
Sababu ya Vikwazo katika malezi ya watoto:-
• Wazazi hawana muda wa kukaa na watoto wao
• Ulaji mbaya unaosababisha udumavu
• Hitaji la kuwa karibu na mzazi uleta mahusiano ya karibu na watoto.
• Kumwacha mtoto mbali na Mama yake mzazi
• Wanaume wameacha/wamejisahau malezi ya karibu na watoto. Inapunguza upendo wa watoto kwa baba.
• Malezi ya kisasa yasiofaa unayompa mwanao (mfano kumpeleka shule yenye kila kitu)
• Changamoto ya "adoption "
• Wazazi kuwa na kazi nyingi
• Ugomvi kati ya Wazazi
• Kuishi na mama wa kambo
• Hisia hasi dhidi ya mtoto kabla hajazaliwa
• Mwonekano wa nje ya wazazi/walezi
• Vyanzo vya elimu kuongezeka mfano TV n.k
1. MALEZI
a. Elimu nzuri ya watoto inaanzia Nyumbani (watoto wenye umri miaka 0-8 walelewa na Wazazi wao). Mtoto asipopata malezi mazuri Nyumbani atakuwa kwa tabia za ajabu.
Mithali 1:8; 6:20-23
Mithali 1:8
Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako
Mithali 6:20
Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako.
Mithali 6:21
Yafunge hayo katika moyo wako daima; Jivike hayo shingoni mwako.
Mithali 6:22
Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda, Na uamkapo yatazungumza nawe.
Mithali 6:23
Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
Kumbuka Mama na baba hawapatikani kule unapompeleka.
Kumb 11:18-19
Kumbukumbu la Torati 11:18
Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu.
Kumbukumbu la Torati 11:19
Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Malezi huanzia Tumboni
Waamuzi 13:7
lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.
Kunyonya uondoa msongo wa mawazo kwa watoto
Mnyonyeshe mwanao maziwa ya kutosha.
Baba kwa watoto
Ukaribu wa baba kwa mtoto unamsaidia kumjengea mapenzi mazuri
Utafiti ulifanywa kwa kuwauliza mbalimbali,
Ukatoa majibu haya kitabu kitabu kinaitwa "Men's against domestic violence"
63% - vijana wenye kesi nyingi, ni wale wanaotoka kwenye familia isiyokuwa na baba
70% - Vijana wenye ualifu katika taasisi za serikali, wanatoka katika familia isiyo na baba
71% - vijana walioacha shule katika level ya secondary wanatoka katika familia isiyo na baba.
75% - vijana wanaoathirika madawa ya kulevya wanatoka familia isiyo na baba
80% - vijana wabakaji, hakuna baba Nyumbani.
85% - walioko magerazani, hakuna
90% - watoto watoro shuleni. Hawana baba nyumbani
95% - Watoto hawajawahi kuwaona baba zao.
UBAMA
Wapo wababa wana watoto lakini kimwili hawana watoto wao, huu ugonjwa unautwa UBAMA-Ukosefu wa baba maishani una madhara makubwa
Wewe baba leta tumaini kwa watoto wako.
KARIBUNI KESHO SOMO LITAENDELEA.
TUBARIKIWE SOTE
Post a Comment